TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, September 1, 2009

libeneka la tanzanite account ya CRDB

4:00 PM
Habari za kazi ndugu Michuzi,
Natumai unaendelea vyema kabisa na shughuli za kila siku.Kuna jambo nataka ushirikiano na wasomaji wa blog ya jamii. Mie ni mwanafunzi na nasoma India. kama inavyojulikana India hawaruhusu kubeba boxi ukiwa denti. Hivyo wengi tunategemea pesa za kujikimu kutoka kwa Wazazi/Walezi ama Wafadhili mbalimbali.
Kuna njia nyingi za kutumiwa pesa lakini wengi tuliona ni muhimu kuwa na account ya Tanzanite(CRDB),mwanzoni nilikuwa nasikia watu wengi wakilalamika kwamba account hii inasumbua, haswa linapokuja swala moja kwamba mtu anaambiwa ame overdraw hivyo account yake ina deni.

Kuna watu wameacha kutumia baada ya kuambiwa wana madeni makubwa wanadaiwa. Je, naomba kuuliza kwenye account kukiwa na millioni 1 bank inaweza kukupa millioni 2? haswa ukifikiria huduma yenyewe tunatumia ni ya Tembocard?

Kwa kawaida viwango vya makato baada ya Transaction huwa vinajulikana lakini kwa bank hii ya CRDB mwisho wa siku mtu unaona maluweluwe na kweli nami wameniambia wananidai hivyo wamekata pesa zote ambazo nilipaswa kupata na bado wanasema nadaiwa 27,000 ya Kitanzania!

Swali muhimu ni hivi Tanzanite account inatakiwa iwe na 5000 rupees ama 100usd na si chini ya hapo?? Je, inakuwaje mtu ana draw pamoja na hizo 5000rupees na zaidi? tuseme machine zina matatizo ama mfumo mzima una matatizo ama wafanyakazi wa CRDB bank wana mbinu zao?

Maana kama mchezo ni huu watakuwa wanatumaliza sie vijana tunaotoka familia za chini. Je wadau tuendelee na Huduma hii ama turejee kwenye West union,money gram ama bank zingine za kimataifa kukwepa hatari hizi?
Mdau aliyelizwa India

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA