TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, September 19, 2009

Kikwete, Sitta, Jaji Ramadhan kushiriki mchezo wa kikapu

11:59 AM

Na Imani Makongoro

VIONGOZI wakuu wa mihimili mitatu ya dola nchini, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Jaji Mkuu, Agustino Ramadhan watapata nafasi pekee na nadra ya kuonyesha vipaji vyao vya kucheza mpira wa kikapu.

Wakuu hao wamealikwa katika tamasha la Siku ya Mchezo wa Mpira wa Kikapu wa Hisani (Basketball Charity Day), ambao umeandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF).

Mchezo utakaofanyika Oktoba 24 kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam huku ukiwa na lengo la kuchangia, kukuza na kuendeleza maendeleo ya mchezo nchini.

Mbali na Rais Kikwete ambaye pia ni mpenzi mkubwa wa mchezo wa kikapu alioucheza wakati wa ujana wake, viongozi wengine wa ngazi za juu wakiwamo mabalozi na viongozi wa makampuni na mashirika mbalimbali ya ndani ya nje ya nchi watashiriki katika mchezo huo.

Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Jaji Mkuu, Agostino Ramadhan wametajwa na waandaaji wa mchezo huo kuwa watakuwa washiriki ambapo siku hiyo wataonyesha mfano kuwa hawako mbali katika shughuli za michezo.

Makamu wa Rais wa TBF, Musa Mziya aliwambia waandishi wa habari kuwa hiyo itakuwa ni changamoto katika mchezo huo, ambapo viongozi wa ngazi za juu wa mihimili hiyo mitatu ya dola wamejitokeza kushiriki.

Alisema, mchezo huo unalenga zaidi katika kupata wachezaji wengi ambao watacheza anga za kimataifa, pia kujenga na kuchangia maendeleo ya mchezo huo ambao unakua kwa kasi nchini .

Alisema Watanzania wenye mapenzi mema na mchezo huo wanakaribishwa kujumuika pamoja siku hiyo ili kucheza mchezo wa hisani katika kuenzi na kuchangia maendeleo yake.

Aliongeza kuwa siku hiyo wanategemea kuamsha ari na nguvu zaidi katika anga za michezo hasa katika mchezo wa kikapu kwani wanategemea tamasha hilo litakuwa kubwa.

Aidha, Mziya aliwaomba wadau, mashirika na watu binafsi kujitokeza kwa wingi zaidi kushiriki katika mchezo huo wa hisani wa kuchangia maendeleo ya mchezo nchini ikiwa ni tamasha la kwanza la aina yake kuwahi kufanyika na kushirika viongozi hao waandamizi.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA