TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, September 5, 2009

JK: Benki ya Wanawake si duka la mjomba

2:30 PM

Rais Jakaya Kikwete, amezindua Benki ya Wanawake Tanzania na kuwaonya viongozi wake wasiiendeshe kama duka la mjomba kwa kutoa mikopo isiyolipwa ili iweze kudumu.

Rais Kikwete, alizindua benki hiyo iliyopo Mtaa wa Mkwepu jijini Dar es Salaam katika hafla iliyohudhuriwa na watu mbalimbali akiwamo mkewe, Salma, mawaziri, wabunge, makatibu wakuu na wawakilishi wa taasisi za kimataifa. Alisema viongozi wa benki hiyo wanapaswa kuiendesha kisasa na kuhakikisha kila anayekopa analipa tena kwa wakati.

"Wekeni sera ya mikopo iliyo nzuri na kila anayekopa arejeshe, acheni kukopesha kama hisani na kusema huyu mwenzetu, huyu wifi huyu tunamjua..Mkifanya hivyo, hamtafika mbali," alisema.

Alisema ingawa Serikali imeipa Benki hiyo Sh. bilioni 2.9, kila mwaka itakuwa ikitenga fedha kwa ajili ya kuijengea uwezo ili iweze kusambaa nchi nzima na kuwa mkombozi kwa wanawake. Rais Kikwete alisema wakati wa kutoa mikopo benki hiyo iweke kipaumbele zaidi kwa wanawake ili waweze kujikwamua na umaskini.

Alisema serikali inawajali na ina dhamira ya dhati ya kumwendeleza mwanamke na kuwaasa kuwa mstari wa mbele kufungua akaunti na kuweka fedha zao kwenye benki hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Margaret Sitta, alimsifu Rais Kikwete kwa kuwajali wanawake na kuwateua katika nafasi mbalimbali za kiutendaji.

Waziri Sitta alisema ushahidi wa hilo ni uteuzi wa majaji 10 alioufanya mwaka jana, kati yao saba walikuwa wanawake, Naye Mkurugenzi wa Benki hiyo,Magreth Chacha, alisema tangu ianze kufanya kazi Julai, mwaka huu, wateja ,1646 wame fungua akaunti, kati yao asilimia 81 ni wanawake na wanaume ni asilimia 19 tu. Chacha alisema benki hiyo ina mpango wa kutumia teknolojia ya kisasa kama vile matumizi ya ATM na Swichi ya Umoja ambayo inamtandao wa benki saba nchini.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA