
Kiasi cha dola milioni 500 kitatumika kutunisha mfuko wa fedha za kigeni wa Zimbabwe ambao umekuwa mtupu kwa kipindi kirefu.
Fedha hizo zitatolewa kwa masharti kuwa waziri wa fedha wa Zimbabwe atahakikisha kuwa hazitumiki kwa miradi isiyokusudiwa.
Zimbabwe inahitaji kuujenga upya uchumi wake ambao umeangamia kutokana na nchi hiyo kuwekewa vikwazo kuibana serikali ya rais Robert Mugabe.
Hatua hiyo imefungua migawanyiko mipya katika serikali ya umoja ya Zimbabwe.
Chama cha MDC kilichowahi kuwa cha upinzani kimekosolewa na rais Mugabe kwa kushindwa kuchukua hatua za kutosha kupata wahisani kuisaidi nchi hiyo.
Kwa upande mwingine, MDC imekishutumu chama cha Zanu-PF kuendeleza vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
0 comments:
Post a Comment