.jpg)
Wavuvi watatu wanahofiwa kufa maji baada mtumbwi waliokuwa wakiutumia wakati wa kuvua samaki kuzama kufuatia kupigwa na upepo mkali.
Kamanda wa Mkoa wa Mwanza Jamal Rwambow ameiambia Alasiri kwa njia ya simu kuwa tukio hilo limetokea hivi karibuni, majira ya saa 5:00 usiku katika kambi ya uvuvi ya Migogo wilayani Sengerema.
Amesema wavuvi hao walikuwa kwenye mtumbwi wa kasia ambao haukuwa na namba za usajili.
Amewataja wavuvi wanaohofiwa kufa kuwa ni Marando, 43 ambaye anatokea eneo la Nyasake, Nagh'oyo, 30 kutoka Geita, Mseneku Kisena, 39 naye kutoka Geita. Amesema mvuvi mmoja Maulid Masudi wa Igoma, Mwanza aliokolewa akiwa hai.
0 comments:
Post a Comment