TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, August 27, 2009

Serikali kununua `bajaji` za kubebea wagonjwa

10:04 PM

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, inatarajia kununua magari ya kubebea wagonjwa ya magurudumu matatu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha huduma za tiba nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Prof. David Mwakyusa, wakati alipokuwa akimkaribisha Naibu Waziri wa Afya toka Australia, Dk. Kim Hames Mla, ambaye ametembelea nchini.

Waziri Mwakyusa akasema kuwa Tanzania imeamua kununua vyombo hivyo ili kuwasaidia wagonjwa wanaotakiwa kupata huduma ya haraka na pia kumfanya mgonjwa awe katika mazingira mazuri ya kulala kwenye kitanda.

“Vyombo hivi vinatumika pia katika nchi za wenzetu kama Malawi... hivyo na sisi tunakazia uzi hapo hapo penye mafanikio,” akasema.

Waziri Mwakyusa akaongeza kuwa, ujio wa Naibu Waziri wa Afya wa Austraria utaweza kutoa nafasi ya kujadili na kutathmini maeneo ambayo yatafaa kushirikiana, ikiwa ni pamoja na yale yahusianayo na matatizo ya wajawazito, watoto wachanga na afya kwa watoto.

Wakati huohuo, Waziri Mwakyusa amesema kuwa Serikali inafanya utaratibu wa kushirikiana na Serikali ya Australia katika nyanja za mafunzo na rasilimali watu pamoja na kutembeleana ili kuweza kujadili mambo mbalimbali ya kiafya.

Waziri pia ameiomba Serikali hiyo kuiwezesha Tanzania kununua magari matatu ya wagonjwa.

Naibu Waziri huyo ameipongeza Serikali kwa kutoa mafunzo na kuajiri wauguzi wengi, ikiwa ni njia mojawapo ya kutoa huduma bora kwa wagonjwa, hasa watoto na akina mama wajawazito.

Aidha, amekiri kuwa Tanzania ina hospitali kubwa ya taifa ukilinganisha na hospitali ya taifa ya kwao.

Dk. Kim na ugeni wake, wametembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chuo cha Udaktari na pia Hospitali ya Amana.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA