TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, August 19, 2009

Kila Mtanzania kupata chandarua mwakani

12:26 AM

Watanzania wote wataanza kupatiwa chandarua maalum vya kuzuia na kuua mbu kuanzia mwakani.Hizo ni jitihada za serikali kutokomeza ugonjwa wa malaria, ilitangazwa jana mjini Dodoma wakati Rais Jakaya Kikwete akifanya mazungumzo na ujumbe ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Margaret Chan kwenye Ikulu ndogo, Dodoma.

Ilitangazwa katika mkutano huo kuwa taasisi ya Global Fund imekubali kutoa kiasi cha dola za Marekani milioni 111, ili kununulia vyandarua vyote milioni 17 ambavyo vinahitajika kwa ajili ya kila kitanda katika Tanzania kuwa na chandarua maalum cha kuzuia na kuua mbu.

Kwa sasa chandarua hizo zinatumika nchini lakini zinatolewa kwa wajawazito na watoto wadogo chini ya miaka mitano.

Fedha hizo za kununulia vyandarua hivyo ni mbali na kiasi kingine cha fedha ambacho kitatolewa na taasisi nyingine kama vile Bill and Melinda Gates Foundation na Clinton Foundation katika kupambana na magonjwa mbali na hasa malaria.

Ugonjwa wa malaria ndio unaendelea kuua Watanzania wengi zaidi kuliko ugonjwa mwingine kila mwaka na kusababisha hasara nyingine nyingi zikiwamo za kiuchumi.

Maeneo makubwa yanayosumbuliwa na ugonjwa wa malaria ni mikoa mitatu inayozunguka Ziwa Victoria ya Kagera, Mwanza na Mara pamoja na wilaya 27 zilizoko katika ukanda wa pwani kuanzia kwenye Mkoa wa Kilimanjaro hadi Mkoa wa Mtwara.

Mbali ya Dk. Chan, ujumbe huo mzito ulikuwa ni pamoja na Dk. Ray Chambers ambaye ni Balozi wa Umoja wa Mataifa katika mapambano dhidi ya malaria na Dk. Yamada ambaye ni mwakilishi wa taasisi ya Bill and Belinda Gates Foundation.

Dk. Chan ameupongeza uongozi wa Rais Kikwete na serikali yake kwa juhudi kubwa za kupambana na kujaribu kuutokomeza ugonjwa wa malaria.

Kwa upande wake, Rais Kikwete alijibu:

“Niko tayari kufanya lolote katika kuongeza mapambano dhidi ya malaria ili mradi msaidie juhudi zetu kwa kutuwezesha na raslimali muhimu katika mapambano hayo.”

Akizungumzia matumizi ya dawa ya kunyunyizia ya DDT ambayo ilifanikiwa kutokomeza malaria katika sehemu mbalimbali duniani, Dk. Chan alisema anaamini kuwa dawa hiyo inaweza kutumika kwa uangalifu katika mazingira fulani fulani kwa kutilia maanani umuhimu wa kulinda mazingira.


1 comments:

Anonymous said...

Asante sana!Nilihitaji kusoma kuhusu malaria kwa madarasa ya Kiswahili.
mwanamaji Ksenia

Post a Comment

 
BONYA HAPA