Na James Magai
BAADA ya kuisubiria kwa muda wa siku 21, hatimaye hukumu ya kesi ya mauaji iliyohusisha askari wa Jeshi la Polisi na kuvuta hisia za wengi, itasomwa leo.
Kutoka jijini Dar es salaam, Mahenge mkoani Morogoro hadi mikoa mingine yote, masikio ya wengi yatakuwa kwenye hukumu ya kesi ya tuhuma za mauaji ya wafanyabiashara watatu wa Mahenge na dereva teksi wa jijini Dar es salaam.
Katika kesi hiyo, ambayo imekuwa ikivuta watu wengi kwenye chumba cha Mahakama Kuu jijini Dar es salaam, polisi tisa, akiwemo mkuu wa zamani wa upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe wanatuhumiwa kuwaua wafanyabiashara hao wa madini ya rubi na dereva teksi.
Jaji Salum Masatti ndiye atakayetegua kitendawili hicho baada ya mapambano ya kisheria ya zaidi ya mwaka mmoja baina ya mawakili wa pande zote mbili, tangu kesi hiyo ilipoanza rasmi kusikilizwa Mei 28, 2008.
Zombe na wenzake wanatuhumiwa kuwaua kwa kukusudia Sabinus Chigumbi, maarufu kama Jongo na ndugu yake Ephrahim Chigumbi na Mathias Lunkombe ambao ni wafanyabiashara wa Mahenge. Mwingine ni dereva teksi wa Manzese jijini Dar es salaam, Juma Ndugu.
0 comments:
Post a Comment