TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, August 27, 2009

Hospitali ya Aga Khan Dar kupima kisukari bure

8:16 AM
Na Fredy Azzah

HOSPTALI ya Aga Khan ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kutoa bure huduma za ushauri na kupima ugojwa wa kisukari kwa kipindi cha siku kuanzia Agosti 29 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam jana, Mtaalamu wa magonjwa yasiyoambukiza katika hospitali hiyo, Dk Liwayway Hussein, alisema uamuzi huo unatokana na kasi ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoumwa ugonjwa huo.

Alisema katika siku ya kwanza,uchunguzi utafanyika Mlimani City, kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.

Alisema Septemba 4 uchunguzi utafanyika katika eneo la Kivukoni Feri kwa muda kama utakaoutumika katika siku ya kwanza huko Mlimani City.

Kwa mujibu wa Dk Hussein, siku ya mwisho,huduma hiyo itafanyika katika Hospitali ya Aga Khan kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 11 jioni.

“Tumeamua kuipeleka hospitali yetu mitaani karibu na watu kwa sababu tunataka watu wajue afya zao, ili tujaribu kupunguza makali ya ugonjwa huu, zamani tulifikiri kuwa ugonjwa upo katika nchi tajiri na kwa watu wazima lakini, kutokana na mfumo wa maisha tunayoishi kila mtu anaweza kuugua kisukari,” alisema Dk Hussein.

Alisema kama mtu akijigundua mapema kuwa na dalili za ugonjwa huo, anaweza kujizuia kuupata.

Dk Hussein alitaja, baadhi ya sababu za ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kutofanya mazoezi ya mwili mara kwa mara na kula vyakula vyenye mafuta mengi, vinavyoongeza uzito kupita kiasi.

Afisa masoko na msemaji wa hosptali hiyo, Eugenia Chanda, alisema huduma hiyo itatolewa bure na kwamba ni moja ya njia za kuisaidia jamii ya Kitanzania katika kupunguza tatizo la ugonjwa wa kisukari.

Kwa mujibu wa Chanda hii ni mara ya pili kwa Hosptali ya Aga Khan, kutoa huduma za afya bure, mara ya kwanza ikiwa ni June mwaka huu, ilipotoa huduma ya mifupa kwa zaidi ya wananchi 200.

“Kwa sasa hosptali imeanzisha utaratibu wa kutoa huduma za kliniki za magonjwa mbalimbali bure angalau kwa siku kadhaa kwa kila mwezi, na katika huduma hizi hakuna mtu atakayetoa hata shilingi kumi," alisema.



0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA