TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, August 12, 2009

Clinton kukutana na viongozi wa Nigeria

6:18 PM

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Bi Hillary Clinton amewasili nchini Nigeira akiwa katika hatua yake ya tano ya ziara ya kutembelea mataifa saba ya bara la Afrika.

Wakati wa ziara yake hiyo ya saa 36 Bi Clinton atakutana na waziri mwenzake wa Mambo ya nje wa Nigeria, Ojo Maduekwe na baadae atafanya mazungumzo na Rais Umaru Yar'Adua.

Wachambuzi wa mambo wanasema waziri huyo wa Marekani atakuwa mkali katika suala zima la rushwa na mageuzi yanayosimamia uchaguzi.

Mwezi uliopita Rais wa Marekani Barack Obama aliiruka Nigeria wakati wa ziara yake ya kwanza rasmi barani Afrika kutokana na kile kilichoonekana rekodi mbovu ya utawala bora.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA