TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, December 10, 2009

Obama apokea tuzo ya amani ya Nobel

11:52 PM

Rais Barack Obama wakati akipokea tuzo ya amani ya Nobel, amesema Marekani lazima ionyeshe wajibu wa nia njema wakati inapopigana vita ambavyo ni lazima na vyenye kufuata sheria.

Katika hotuba yake mjini Oslo, Obama alitetea wajibu wa Marekani katika vita vya Afghanistan, akisema kwamba nguvu za kijeshi zaweza kuleta amani ya kudumu.

Alisema amepewa tuzo hilo mapema ukilinganinishwa na watu wengine walioshinda tuzo hilo kabla yake.

Akizungumza kwa unyenyekevu, alisema wengine walistahili zaidi. Bw Obama pia alizungumzia vita viwili vinavyoongozwa na Marekani, akisema kuwa anafahamu kabisa gharama za vita hivyo.

Bw Obama alishinda tuzo hiyo mwezi Oktoba mwaka huu "kwa jitihada zake za kipekee kuimarisha diplomasia ya kimataifa na ushirikiano katika ya watu".

Sherehe hizo za siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Norway zilifanyika siku chache baada ya Bw Obama kutangaza kuongezwa kwa wanajeshi zaidi 30,000 kwenda nchini Afghanistan.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA