Kijana mmoja mkazi wa Jijini Dar es Salaam, amekufa papohapo baada ya kujilipua kwa risasi leo asubuhi.
Kijana huyo amefahamika kwa jina la Idd Swaibu Hoza, 28, mkazi wa Mbezi Ndumbwi.
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Ndumbwi, Bw. Salustian Cashimiry Kimaro ameliambia gazeti hili leo asubuhi kuwa, tukio hilo limetokea mishale ya saa 3:00 asubuhi, nyumbani kwa wazazi wa mwanafunzi huyo maeneo ya Mbezi.
Akisimulia tukio hilo, Bw. Kimaro amesema kijana huyo alitarajia kuanza masomo ya elimu ya juu hivi karibuni, baada ya kumaliza kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa.
Amesema bunduki aliyotumia ni aina ya Shortgun na hutumiwa na mlinzi anayelinda nyumbani kwao.
Amesema mlinzi huyo aitwaye Eliud Seleman Ntaita kila siku anapomaliza lindo lake, huhifadhi silaha hiyo chini ya uvungu wa kitanda nyumbani hapo na kisha huondoka zake.
Bw. Kimara amesema hadi sasa sababu za kijana huyo kujilipua bado hazijafahamika.
0 comments:
Post a Comment