Viongozi wa ile taasisi ya kupanda na kuvuna fedha ya Development Enterprenureship Community Initiative, DECI, inayodaiwa kuendesha shughuli za upatu kinyume cha sheria za nchi, wamekwaa kesi mpya.
Hati ya mashtaka ya kesi hiyo, inawataja washitakiwa kuwa ni Dominic Kigendi, Jackson Sifael Mtalesi, Timotheo Ole Loiting'ye na Samwel Mtalesi.
Wote wanashitakiwa kwa kosa la wizi.
Hati ya mashtaka inasema, watuhumiwa hao wakiwa wakurugenzi wa DECI Tanzania Ltd, kati ya Desemba Mosi na Desemba 8 mwaka huu, wakiwa mahali pasipojulikana, walikula njama kwa nia ya kuibia umma kiasi cha shilingi 118,440,000.
Katika kosa la pili, watuhumiwa wote wanadaiwa kuwa mnamo Desemba 8 mwaka huu, wakiwa katika Benki ya Standard Charterd tawi la Kariakoo, Ilala Jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walikuwa na lengo la kuiba shilingi 118,440,000, mali ya kampuni ya DECI.
Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, watuhumiwa hao waliofikishwa kwenye mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu mapema asubuhi, walikuwa bado hawajapandishwa kizimbani.
0 comments:
Post a Comment