 |
| Mwili wa marehemu. |
 |
| Umati uliokuwa kwenye tukio. |
 |
| Wananchi
wa maeneo hayo wakiangali huku wakijiuliza maswali ya kwanini matukio
ya kujichukulia sheria mikononi bado wanaendekezwa na Wananchi. |
 |
| Koki aliyokutwa nayo marehemu Hassan Stanley. |
 |
| Mwandishi
wa habari Fabian Fanuel kutoka FPLUSS BLOG akiwa na Mwandishi wa
habari wa Kwaneema Fm Joshua Dede wakimhoji mwenyekiti wa mtaa wa
Chanmwenda bi. Lucy Kapombe. |
 |
| Mwenyekiti
wa Mtaa wa Kiloleli bwana Joshua Josia Mnana akiwatoa maelezo mbele ya
waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kifo cha Hassan Stanley. |
 |
| Huwezi
amini unachokiona hiki ni kinyesi alichojisaidia Hassan baada ya
kuchomwa moto hadi kupelekea umauti wake alfajiri ya leo katika uwanja
wa mbuzi Kiloleli Mwanza. |
 |
| Kaka yake Marehemu Hassan akimfunika kanga mdogo wake baada ya kukutwa na tukio la kuuawa kwake.. |
 |
| Mwili wa marehemu Hassan Stanley akiwa amefunikwa kanga na kaka yake. |
Kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina la Hassan Stanley asubuhi ya kuamkia leo
majira ya saa kumi na moja katika maeneo ya uwanja wa mbuzi Kiloleli
jijini Mwanza, ameuawa na wananchi wenye hasira kali kwa kupigwa na
kuchomwa moto hadi kupelekea mauti yake.
Akiongea na mtandao wa fpluss.blogspot.com
Mwenyekiti wa mtaa wa maeneo tukio lilipotokea Bi Lucy Kapombe amesema
kuwa haya ni matokeo na hasira walizokuwa nazo wananchi ambao wamekuwa
wakilalamikia matukio ya wizi wa koki za maji maeneo mbalimbali katika
jiji la Mwanza.
Amesema
yeye binafsi hauingi mkono mwizi yeyote kuuawa bali wananchi wanatakiwa
kuiacha sheria ifuate mkondo wake katika watuhumiwa wanaokuwa
wamekamatwa kutokana na matukio mbalimbali ya uhalifu katika jamii yetu.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa mtaa wa Kiloleli b bwana Joshua Josia Mnana
ameto wito kwa vijana wanohusika katika uhalifu mbalimbali kuacha ili
wasije wakapatwa na matukio kwa hayo yaliyompata mwenzao.
Marehemu
Hassana Stanley aliye na umari wa kati ya miaka 22 hadi 26 alikuwa
mpiga debe katika kituo cha Kiloleli na ni kazi ambayo amekuwa akiifanya
mpaka anakutwa na umauti.
Mtandao wa fpluss.blogspot.com unalaani matukio ya wananchi kujichukulia sheria mikononi mwao.
KWA HISANI YA B PLUSS BLOG
0 comments:
Post a Comment