TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, March 12, 2012

Uganda yashuhudia wakimbizi wanaokimbia mapigano nchini DRC

11:44 AM
wakimbizi kutoka Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kwamba zaidi ya watu 100,000 hadi sasa wamelazimika kuhama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati mapigano kati ya makundi hasimu yaliyojihami yanapoendelea kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Mapigano kati ya vikosi vya serikali na kundi la FDLR yalichacha mwezi Novemba mwaka uliopita na kusababbisha kuhama kwa maelfu ya watu.
UNHCR inasema kwamba kwa mwaka huu pekee zaidi ya watu 3000 wameukimbia mkoa wa Kivu Kaskazini na kuingia magharibi mwa Uganda wakikimbia mapigano hayo. Adrian Edwards kutoka UNHCR anasema kwamba kuna ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu uliotendwa na makundi hayo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA