Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassin Ng’amilo akifafanua jambo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana juu ya utekelezaji wa mradi uwekaji boya jipya la mafuta.
TAARIFA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MRADI WA UJENZI NA UWEKAJI WA BOYA JIPYA LA MAFUTA (SINGLE POINT MOORING – SPM)
UTANGULIZI
Mradi wa ujenzi uwekaji wa boya jipya la kupakulia mafuta yaliyosafishwa (white products) na yasiyosafishwa (crude oil), ulitiwa saini kati ya Mkandarasi “M/s. Leighton Offshore Pte mwenye makao makuu Singapore na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) tarehe 30 Septemba 2010. Mradi huu ambao unategemewa kukamilika mwezi April 2012 utagharimu kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 70 (sabini) kwa pesa za TPA na mkopo kutoka Benki ya CRDB.
Mradi utakapomalizika utaongeza uwezo wa upakuzi wa mafuta kutoka meli za ujazo wa 40,000 kufikia meli zenye ujazo wa tani 150,000 (Laki moja na hamsini) katika kina cha maji chenye urefu wa mita 25. Boya linalowekwa litakuwa na mabomba mawili, moja la inchi 28 kwa ajili ya mafuta meusi (crude oil) na la pili inchi 24 kwa ajili ya upakuaji wa mafuta yaliyosafishwa (petrol, diesel, kerosene, JetA1) ambayo yatatambaa kupitia chini ya Bahari kwa takribani km 3.6 na km 4.3 chini ya ardhi hadi Kigamboni ambapo bomba la mafuta meusi litaelekezwa TAZAMA na la mafuta yaliyosafishwa litaendelezwa mpaka kwenye matanki ya kuifadhi mafuta kwa muda (custody transfer tanks) itakayojengwa Kurasini karibu na Dock yard. Endelea
|
Friday, January 27, 2012
0 comments:
Post a Comment