Ni
Shirika letu la ndege la Taifa (ATC). Lilianzishwa mwaka 1973 likiwa na
ndege 11. Kwa sasa hata hivyo hakuna hata ndege moja inayofanya kazi.
Tatizo
hasa la Shirika hili ni nini? Kwa nini Precision ifanye vizuri hivi na
shirika la taifa lishindwe? Na bado serikali iko katika mchakato wa
kulimwagia "vitendea kazi na mtaji" mpya. Shirika hili litaendelea kutafuna mabilioni ya walipa kodi mpaka lini? Kwa nini tunazidiwa hata na vinchi vidogo kama Burundi na Rwanda? |
0 comments:
Post a Comment