Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM limetuma boti yake ya pili
nchini Libya kwa ajili ya kuwakwamua wahamiaji waliokwama kwenye eneo
hilo kufuatia mapigano ambayo sasa yamefikia kwenye kitovu cha kuangusha
utawala wa Gaddafi. Boti hiyo imeanza kuondoka toka katika mji wa
Benghazi ulioko kaskazini mwa Libya na kuelekea katika mji mkuu Tripoli.
Ndani yake imesheheni huduma mbalimbali ikiwemo madawa, huduma za
dharura pamoja na mahitaji mengine muhimu. Zaidi ya wafanyakazi 50
wameambatana na boti hiyo kwa ajili ya kutoa misaada ya kibinadamu. Boti
hiyo inatazamiwa kutia nanga mjini Tripoli mwishoni mwa juma hili
(JUMBE OMARI JUMBE NI MSEMAJI WA IOM) |
0 comments:
Post a Comment