Umoja wa Mataifa umelaani vikali mashambulizi yaliyolenga majengo ya
umoja wa mataifa nchini Nigeria ambako watu kadhaa walipoteza maisha na
wengine kujeruhiwa. Bomu hilo lilitengwa kwenye gari lililipukia jengo
la umoja wa mataifa lililoko kwenye mji mkuu Abuja ambako kunapatikana
ofisi kadhaa za mashirika ya umoja wa mataifa.
Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
amesema kuwa kitendo hicho ni dhihaka dhidi ya watu waliojitolea kwa
ajili ya kuwasaidia watu wengine.
Amesema amemtuma msaidizi wake Asha-Rose Migiro kuelekea nchini humo kwa ajili ya kuangalia athari zake.
(SAUTI YA BAN) |
0 comments:
Post a Comment