TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, July 20, 2011

Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006) Danny Mwakitereko Apata Ajali Jijini Dar es Salaam

11:03 PM

Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New habari (2006) Danny Mwakitereko(Pichani juu) amepata ajali ya gari jana usiku, jijini  Dar es Salaam.Amefanyiwa upasuaji wa kichwa,katika Taasisi ya mifupa Muhimbili,sasa yuko ICU Muhimbili kama anavyoonekana kwenye picha hapo juu leo hii.Tumwombee ndugu yetu Mungu amponye haraka ili tuungane naye katika kusukuma gurudumu la maendeleo kwa manufaa ya taifa.
By Arodia
Journalist, Mtanzania.
 --
Jumbe Mbalimbali Kutoka Kwa  Wahariri Wa Vyombo Vya Habari walioshuhudia hali Leo Hii yake Zinasema Hivi..:

Jesse Kwayu 
    
Wandugu, nimetoka MOI hivi punde. Nimefanikiwa kumwona Danny tulifuatana na Jabir. Hali yake kwa mujibu wa wataalam wa tiba ni nzuri. Amefanyiwa upasuaji sehemu ya kichwa kwenye paji la uso. Vipimo vimeonyesha kwamba hakuna tatizo lingine kubwa ndani ya kichwa. Anaweza kupumua mwenyewe bila msaada wa mashine, ingawa wataalam wameamua kumwekea mashine ili asichoke.

Kimsingi bado hali yake ni serious, lakini kitabibu amepiga hatua kubwa ya kupata nafuu.


Theophil Makunga    

Ndugu zangu, ndiyo kwanza nimefika ofisini nikitokea kumwangalia Danny.
    
Ndugu zangu, ndiyo kwanza nimefika ofisini nikitokea kumwangalia Danny. Kwa kusena ukweli mwenzetu ameumia. Kwa sababu ndiyo kwanza alikuwa ametoka theatre, unamwangalia tu akipumua kwa msaada wa mashine. Kichwa kimevimba kiasi kwamba  si rahisi kumtambua kuwa ni Danny.

Kwa maelezo ya nesi, hakuna sehemu nyingine zaidi ya kichwa aliyoumia. Kila mmoja wetu kwa dini anayoamini, tusali mungu amsaidie kupambana na maumivu aliyonayo.

Kuhusu ombi la Mwitumba mpaka sasa hakuna anayefahamu hasa ajali ilivyokuwa ila taarifa nilizonazo ni kwamba alikuwa peke yake kwenye gari akitokea ofisini kwenda nyumbani na alipata ajali maeneo ya TIOT Mandela road karibu na daraja baada ya kupita ofisi za Mwananchi kuelekea Tabata Dampo ukitokea Ubungo. Aliwasiliana na mkewe kuwa alikuwa anakwenda nyumbani na baada ya muda mrefu kupita mkewe alipoona hajafika nyumbani aliamua kumpigia simu ikapokelewa na mtu ambaye alijieleza kuwa alimwokota kwenye mtaro baada ya kupata ajali na alikuwa naye hospitalini wengine wanasema Mwananyamala lakini wengine wanasema Amana. Details za ajali hiyo mimi bado sijapata. Tumwombee Mungu amsaidie apone haraka.

Makunga

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA