TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, July 21, 2011

Majibu ya Hoja ya Waziri wa Habari Zanzibar katika Baraza la Wawakilishi.

6:24 PM

NA   YUSSUF SIMAI 

MAELEZO ZANZIBAR        21/7/2011
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Abdilahi Jihadi Hassan amesema kuwa  Wizara yake itajitahidi  kuimarisha Shirika la utangazaji Zanzibar kwa kujitahidi kuipatia Vitendea kazi vya kisasa.

Amesema kuwa kwa hivi sasa tayari Mitambo ya Digital  ya Television Zanzibar mengi imeshawasili Zanzibar kwaajili ya kazi hiyo ya ufungaji. Waziri Jihadi amesema hayo wakati alipokuwa  akijbu hoja za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar juu  ya michango ya wizara yake.

Amesema kuwa Wizara yake inatarajia kuanzia tarehe 25 mwezi huu kufunga Mitambo hiyo Unguja na Pemba.Akizungumzia juu ya suala la kuzimika kwa matangazo ya Sauti ya Tanzania Zanzibar na Television Zanzibar mara kwa mara amesema kuwa hilo ni tatizo la umeme na pia kutopatikana kwa mafuta ya Jenereta katika vituo hivyo kwa ufinyu wa bajeti.

Mhe Jihadi amesema kuwa maslahi ya Wafanyakazi wa Vyombo vya Habari tayari  yamezingatiwa na Serikali kuu. Hata hivyo Wizara bado inawasaidia wafanyakazi wake katika kuwapatia posho zaidi wanapokuwa katika kutekelkeza kazi za Baraza La wawakilishi.

Juu ya Wadaiwa Sugu katika Hoteli ya Bwawani amesema kuwa kwa ujumla wapo wadaiwa watano ndio Sugu kati ya wadaiwa kuminatatu na hao watano wamearifiwa lakini mpaka sasa bado hawajalipa na Mawasiliano bado yanaendelkea.

Waziri Jihadi amesema kuwa Serikali mpaka sasa haina mpango wakuibinafsisha Hoteli hiyo isipokuwa hivi sasa imo mbioni kuimarisha hoteli hiyo  na ndio maana Wafanyakazi wote walioajiriwa wanalipwa na Wizara yake.

 Akielezea juu ya hali mbaya ya Makumbusho ya Mnazi Mmoja  amesema kuwa Makumbusho hayo hivi sasa yameshaanza matengenezo kupitia Mradi wa MANCEP na baadae hatuwa nyengine za uboreshaji zitafuata.

  Juu ya kuharibika kwa viwanja vya Amaan,Mao tse tung na Gombani Pemba amesemna kuwa tatizo kubwa lakuharibika kwa uwanja wa Amaan ni kutumika katika shughuli za Sherehe mbali mbali za Serikali  lakini tayari Wizara yake imeshaanza utaratibu wa matengenezo wa Uwanja huo.

Juu ya hali ya uwanja wa Mao tse tung amesema kuwa uwanja huo umekabidhiwa kwa chama cha mpira wa miguu Zanzibar ZFA ,hata hivyo wizara yake imo katika hatuwa za kuangalia tena utaratibu wa uwendeshaji uwanja huo  .Mheshimiwa Abdillahi Jihad Hassan ameendelea kusema kuwa Majani  ya Uwanja wa Gombani Pemba yanatarajiwa kufika hivi karibuni na  mara baada yakufika majani hayo yatawekwa uwanjani hapo.

Baada ya majadala makubwa nakukubaliana baadhi ya mambo kufuatiliwa yakliwamo Ununuzi wa Mitambo ya Digital wa Television Zanzibar na Mkataba wa Kisiwa cha Changuu nakuwasilisha ripoti hiyo katika kikao kijacho cha Baraza la Wawakilishi baadae Kamati ya Baraza la Wawakilishi  lilipitisha Makadirio  Mapato na Matumiuzi ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar kwa kipindi cha fedha cha miaka 2011/2012.

Jioni Wizara ya Mifugo na Uvuvi ilitarajiwa kusoma hotuba yake ya makadirio ya Fedha kwa kipindi cha mwaka 2011/2012.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA