TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, July 24, 2011

JK Mgeni Rasmi Siku Ya Mashujaa

7:50 PM
NA JOSEPH ISHENGOMA
MAELEZO, MTWARA
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete keshokutwa (25/07/2011) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kumbukumbu ya Mashujaa itaayofanyika kitaifa Naliendele, Mtwara.
 
Kwa mujibu wa ratiba ya Maadhimisho iliyotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Rais akiwa katika uwanja wa kumbukumbu ya mashujaa wa Naliendele, atawaongoza viongozi wenzake kuweka silaha za asili katika mnara wa mashujaa.
 
Ratiba hiyo inaonyesha kuwa Rais ataweka Mkuki na ngao, wakati Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na usalama ataweka sime. Kiongozi wa Mabalozi nchini ataweka shada la maua, Meya wa Manispaa ya Mtwara- Mikindani ataweka upinde na mishale na Mwenyekiti wa Tanzania Legion ataweka shoka.
 
Baada ya tukio hilo, kutakuwepo na sala kutoka kwa viongozi wa dini akiwemo Sheikh kwa niaba ya Waislam, Mchungaji kwa niaba ya C.C.T na Padre kwa niaba ya Roman Cathoric.
 
Aidha gwaride la majeshi ya ulinzi na usalama litatoa heshima kwa Mhe. Rais na kupiga wimbo wa Taifa kabla ya Rais Kikwete kutembelea makaburi na nyumba ya makumbusho ya Naliendele.
 
Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa 3:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA