Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi) akihutubia
katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Nguruka,mkoani Kigoma mwishoni
mwa wiki iliyopita, ambapo aliwaeleza wananchi kutoa ushirikiano kwa
wajenzi wa barabara ya lami ya Malagalasi-Nguruka yenye urefu wa Km 48,
sambamba na ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lenye urefu wa
mita 275

Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila
(kulia),akipongezwa na Diwani wa Kata ya Itebula (NCCR-Mageuzi), Shukuru
Chiza baada ya kuhutubia mkutano wa kuwashukuru wananchi waliompigia
kura katika Kata hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Jimbo, Venance Mwaka.
Mkutano huo ulifanyika katika Kata hiyo mwishoni mwa wiki.

Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kusini,kupitia NCCR-Mageuzi, David Kafulila
(kushoto), akijadiliana jambo na Meneja wa Wakala wa Barabara wa
Serikali (TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku (wa pili kushoto)
pamoja na Katibu wa Mkoa wa Kigoma, Sekulu wakati wa ziara ya ukaguzi wa
ujenzi wa daraja la kihistoria la Malagalasi lililopo katika Jimbo
hilo.

Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (kushoto) akiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu, Joseph Simbakalia (katikati) walipokuwa
wakipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Wakala wa Barabara wa Serikali
(TANROADS), Mkoa wa Kigoma,Haruna Senkuku kuhusu ujenzi wa Barabara ya
kwanza ya lami ya Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo
la Kigoma Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi
huo mwishoni mwa wiki.

Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia (aliyevaa suti
nyeusi) pamoja na vingozi wengine wa mkoa huo akiwemo Mbunge wa Jimbo la
Kigoma Kusini, David Kafulila wakiangalia eneo patakapojengwa daraja
jipya la Mto Malagalasi, walipotembelea eneo hilo hivi karibuni.

Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akimuuliza jambo
Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kusini, David Kafulila (katikati aliyevaa tai)
walipokuwa wakikagua ujenzi wa Barabara ya kwanza ya lami ya
Kidahwe-Uvinza yenye urefu wa Km 76 inayojengwa Jimbo la Kigoma
Kusini,mkoani Kigoma. Viongozi hao wawili walitembelea mradi huo
mwishoni mwa wiki.Picha na Richard Mwaikenda.
0 comments:
Post a Comment