TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Tuesday, May 24, 2011

WASHTAKIWA WA KESI YA EPA WAHUKUMIWA jela MIAKA 5.

11:03 AM


Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein (kushoto) Rajabu Maranda (kulia) Wakiwa ndani ya gari la Polisi tayari kwa safari ya kwenda rumande kutumikia kifingo cha miaka mitano mara baada ya kutoka kwa hukumu yao leo (jana).
Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala Hussein (kushoto) na Rajabu Maranda (kulia) Wakiingia kwenye gari ya Polisi tayari kwa safari ya Rumande.

========= ======= ========
Na Ripota Wetu jijini

Washitakiwa katika kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya
madeni ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Farijala
Hussein na binamu yake Rajabu Maranda, wamehukumiwa miaka mitano jela
ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa Serikali.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na
jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh. Saul Kinemela. Katika mashitaka yao nane yanayowakabili shitaka la kwanza lilifutwa kwa kuwa upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Ilvin Mgeta
alisema wamesikiliza na kuzingatia maombi ya upande wa mashitaka katika
kutoa adhabu hiyo "Kwa kosa la pili mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha
miaka mitatu jela, kosa la tatu na la nne washitakiwa wote watatumikia
adhabu ya miaka mitano, kosa la tano mshitakiwa wa pili pekee atatumikia
adhabu ya miaka miwili jela.

"Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka
miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka
mitatu jela," alisema Hakimu Mgeta.Jumla ya miaka ya adhabu hiyo ni 21, ambapo alisema adhabu hizo zitaenda kwa pamoja hivyo washitakiwa hao watatumikia miaka mitano

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA