Waziri
Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akiwahotubia wakazi wa Manispaa ya
Iringa katika uwanja wa Samora juzi wakati wa harambee ya kuchangia
kituo cha watoto yatima (picha na Francis Godwin).
Na Francis Godwin ,Iringa
WAZIRI
mkuu mstaafu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Frederick Sumaye
ametaja baadhi ya mambo yanayoweza kuvuruga amani ya Tanzania iwapo
hayatashughulikiwa huku akitaka mapamano ya kisiasa yafanyike kwa
umakini mkubwa ili kuepusha vurugu.
Alisema
kuwa amani ni rasilimali kubwa katika nchi yoyote na amani inaweza
kutoweka na kuirudisha kwake ikawa ni kazi ngumu na kwa gharama kubwa
iwapo misingi ya amani katika Taifa isipoheshimiwa na wananchi
wote.
Sumaye
aliyasema hayo jana wakati akichangia kiasi cha shilingi milioni 1
katika katika tamasha la nyimbo za Injili kwa ajili ya harambee ya
kuchangia ujenzi wa kituo cha Teknolojia ya habari na
mawasiliano(ICT)kwa watoto yatima mkoa wa Iringa kupitia kituo cha
Children Care Development Organization (CCDO) iliyofanyika kwenye uwanja
wa Samora mjini Iringa.
Sumaye
aliyataja baadhi ya mambo ambayo yanaweza kuvuruga amani kuwa ni
pamoja na ubaguzi wa aina mbali mbali, chokochoko za kiimani au dini
,mapambano ya kisiasa ,mtawanyiko wa mali au utajiri usiofaa na jambo
jingine ni rushwa na ufisadi.
Hivyo
aliitaka serikali kupambana kwa nguvu zote na vitendo vya Rushwa
na ufisadi na kuwa penye rushwa mwenye haki hunyimwa haki yake stahiki
na kupewa asiyestahiki kwa vile tu kutoa rushwa na kuwa rushwa na
ufisadi vikiendelea kuota mizizi.
Akifafanua
zaidi alisema kuwa chokochoko za kiimani au dini ni jambo la hatari
sana katika nchi yetu na lazima likemewe na lidhibitiwe kwa nguvu zote
kwani ubaguzi wa kidini ukiota mizizi amani huyeyuka kama barafu
iliyoanikwa juani .
Kuhusu
mapambana ya kisiasa Sumaye alitaka vyama kuendelea kupambana kisiasa
huku vikilinda amani na utulivu na kuwa mapambano ya kisiasa
yanahitaji utulivu na kuvumiliana kati ya vyama vinavyopingana ili
visije vikaliingiza Taifa katika kupigana badala ya kupingana .
“…Nasema
katika shughuli za kisiasa lazima taratibu za demokrasia zifuatwe
…shughuli za siasa zifanyike kwa haki na uwazi na wanaoshindwa wakubali
matokeo ya uchaguzi…pia suala la mtawanyiko wa mali au utajiri
usiofaa…kama utajiri wan chi utaonekana umejikusanya kwa wachache na
wengi wamebaki maskini hali ya amani itatoweka bila kujali kama
walio nacho wamepata utajiri wao kihalali au lah …Hali hili kama ipo
lazima irekebishwe na serikali ina taratibu za kufanya marekebisho kama
hayo”
Sumaye
alisema kuwa jambo jingine ambalo ni hatari kwa amani kwa Taifa ni
vitendo ya rushwa na ufisadi ambavyo ni tatizo kubwa linaloweza
kuvuruga amani ya Taifa iwapo haki itaendelea kutendeka kwa watoa
rushwa na mafisadi pekee.
“Lazima rushwa na ufisadi upigwe vita kwa nguvu zote katika nyanja zote za kisiasa ,za huduma au za utoaji haki”.
Hata
hivyo Sumaye alitaka watanzania kujenga moyo wa kuwasaidia yatima
mbali mbali badala ya kuendelea kuongeza nguvu zaidi katika rushwa na
vitendo vya ufisadi ambao ni hatari kwa amani ya Taifa.
Pamaoja
na kumpongeza maratibu wa kituo hicho Majaliwa Mbongella kuwa na wazo
nzuri hilo la kuwajali yatima bado aliwaomba watanzania kujitokeza
kusaidia kituo hicho ambacho kinahitaji kiasi cha shilingi milioni 120
ili kuweza kutimiza ndoto yake ya kujenga kituo hicho cha habari na
mawasiliano kwa yatima.
Awali
mratibu wa kituo hicho Mbogella alisema kuwa kituo hicho kinataraji
kuanza kwa kuwa na matawi mawili moja wilaya ya Makete na taji jingine
mjini Iringa na kuwa kwa lengo ni kuwa na watoto 120 ambao wataanza
kunufaika na mpango huo.
Hata
hivyo alisema kuwa tayari kituo kilichosajiliwa kwa namba
000NGO/00003818/2009 kimepata ardhi zaidi ya ekari 25 katika eneo la
Mkimbizi Iringa mjini 5 na Tanangozi Iringa vijijini 20 na kuwaomba
watanzania wenye mapenzi mema watakaoguswa na maisha ya yatima kuingia
katika blogu ya francisgodwin ama kuwasiliana na yeye (Majaliwa
Mbogella)mratibu kwa namba 0752507519.
Mbogella
alisema kuwa kituo hicho kitakuwa ni baba na mama wa yatima hao na
kuwa mbali ya kuanza na yatima wa Makete na Iringa bado kituo
kitasaidia watoto wa mikoa ya jirani kama Mbeya, Ruvuma ,Morogoro,na
Dodoma ambako baadaye kutajengwa matawi pia.
0 comments:
Post a Comment