Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akiangalia aina mbalimbali ya vitabu vya kufundishia somo la kemia
wakati wa ufunguzi wa mwaka wa kimataifa wa kemia. Waziri Prof. Makame
alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe hizo zilizoandaliwa na
Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya
UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond
Jubilee.
Kakue
Mafole kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa Serikali (kulia) akiwaelezea
waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa
(kushoto) na waziri wa ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dk. Terezya
Huvisa (wapili kushoto) jinsi ofisi hiyo inavyofanya kazi za kupima vitu
mbalimbali. Waziri Prof. Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa
sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es
Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akimshauri Mkuu wa kitengo cha Kemia kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam
Dk. Phillip Joseph jinsi gani wanaweza kufanya kazi ya kuchuja maji
hadi kufikia hatua ya kuwa maji safi na salama kwa ufasaha zaidi na
hivyo kuingia katika soko la ushindani wa biashara. Waziri Prof. Makame
alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa
kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa kushirikiana na
Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika
ukumbi wa Diamond Jubilee.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto)
akimsikiliza Sara Rubagumya (wa kwanza kulia) mwanafunzi wa kidato cha
tatu kutoka shule ya Sekondari Tegeta iliyopo jijini Dar es Salaam
kuhusu jinsi ya kuzalisha umeme kwa njia isiyo na gharama. Waziri Prof.
Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa
kimataifa wa kemia uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa
Diamond Jubilee.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (watatu
kutoka kushoto) akimsikiliza Salim Buyogera mwanafunzi wa kidato cha
sita kutoka shule ya Sekondari Mbeta iliyopo jijini Mbeya alivyokuwa
anaelezea jinsi vipande vya mabati vinavyoweza kuhifadhiwa na kutumika
kufanya mambo mengine wakati wa sherehe za mwaka wa kimataifa wa kemia
uliofanyika leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.
Kushoto kwa waziri ni Naibu waziri wa wizara hiyo Philipo Mulugo na
kulia kwa waziri ni Chande Othman mwenyekiti wa chama cha wakemia
nchini.
Elizabeth
Mlay (kulia kwa waziri ) mwanafunzi wa kidato cha sita kutoka shule ya
Sekondari Jangwani iliyopo jijini Dar es Salaam akimuelezea Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) jinsi
ya kutengeneza dawa ya kusafishia na kuondoa harufu chooni. Waziri Prof.
Makame alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa sherehe za mwaka wa
kimataifa wa kemia zilizoandaliwa na Chama cha wakemia Tanzania kwa
kushirikiana na Kamisheni ya Taifa ya UNESCO uliofanyika leo jijini Dar
es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee.Picha na Anna Nkinda -
Maelezo
0 comments:
Post a Comment