Takriban milipuko mikubwa mitano imeitikisa Tripoli usiku kucha,
wakati harakati za majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato
zikiendelea kwenye mji mkuu wa Libya.
Kwa usiku wa pili, mashambulio ya anga yalilenga ngome ya Bab al-Aziziya ya Kanali Muammar Gaddafi.
Nato inatekeleza azimio la umoja wa mataifa la kulinda raia wa Libya, kufuatia maandamano dhidi ya uongozi wa Kanali Gaddafi.
Lakini Urusi, ambayo haikuunga mkono azimio hilo, imesema uvamizi huo ni ukiukwaji wa umoja huo.
Mwandishi wa BBC Andrew North mjini Tripoli
alisema mashambulio ya Jumanne usiku si makubwa kama yaliyofanyika
Jumatatu usiku, lakini bado yalitikisa majengo eneo kubwa.
Moshi ulionekana kutanda kwenye mji huo.
Nato ilisema ngome hiyo ya Bab al-Aziziya
imekuwa ikitumika kama kituo cha majeshi na magari ya kijeshi
yaliyotumika kushambulia raia.
Lakini serikali ya Libya imesema Nato inajaribu kumwuua Kanali Gaddafi na mashambulio ya usiku yanawatisha raia wa Tripoli.BBC |
0 comments:
Post a Comment