TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Thursday, May 19, 2011

MAKUNDI YA TIMU KOMBE LA DUNIA U-17 KWA WANAUME…!!!

10:21 AM
Kufanyika Mexico City kuanzia June 18 hadi July 10, 2011.
Wenyeji Mexico kufungua dimba na DPR Korea
Mashindano ya Kombe la Dunia kwa vijana wa kiume chini ya umri wa miaka 17 yataanza kutimua vumbi Juni 18 hadi julai 10 mwaka huu nchini Mexico.

Katika mechi ya ufunguzi mabingwa wa kombe hilo wa mwaka 2005 wenyeji Mexico watashuka dimbani kuvaana na timu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (DPRK)katika mchezo wa kundi A utakaopigwa katika mji wa magharibi wa Morelia uliopo jimbo la Michoacan.

Wakati huo ho katika mechi ya ufunguzi ya kundi B wapinzani Ufaransa na Argentina watafundishana soka katika mchezo utakaofanyika Monterrey.

Michuano hiyo itashirikisha nchi 24 ambazo zimepangwa katika makundi sita kama ifuatavyo.:-

  • KUNDI Mexico, DPR Korea, Congo, Uholanzi

  • KUNDI B Ufaransa, Argentina, Japan, Jamaica.

  • KUNDI C Uruguay, Canada, England, Rwanda.

  • KUNDI D Marekani, Jamhuri ya Czech, Uzbekistan, New Zealand.

  • KUNDI E Burkina Faso, Ujerumani, Panama, Ecuador.

  • KUNDI F Australia, Ivory Coast, Denmark, Brazil.

  • MIJI ITAKAYOCHEZEWA
  1. Mechi za kundi A zitachezewa Western City of Morelia in Michoacan.
  2. Mechi za kundi B zitachezewa City of Monterrey.
  3. Mechi za kundi C zitachezewa Central City of Pachuca.
  4. Mechi za kundi D zitachezewa Northern City of Torreon.
  5. Mechi za kundi E zitachezewa City of Guadalajara.
  6. Mechi za kundi F zitachezewa City of Queretaro.
Kundi F limebatizwa jina la ‘kundi la kifo’ likiwa na Brazil ambayo imewahi kuchukua ubingwa huo mara 3.

Afrika inawakilishwa na timu 4 za Burkina Faso, Congo, Rwanda na Ivory Coast.

Mechi ya fainali itachezwa mkubwa sana wa soka wa Azteca uliopo Mexico City mnamo Julai 10, 2011.
Bingwa mpya atakabidhiwa upya kikombe mwaka huu kwa kuwa mabingwa watetezi wa mwaka 2009 Switzerland hawakufanikiwa kufuzu kwa fainali za 2011 nchini Mexico.

1 comments:

emu-three said...

SIE KAZI YETU NI KUTIZAMA NA KUCHEZEA MDOMONI, SIO MBAYA, KWANI IPO SIKU TUTALICHUKUA KOMBE

Post a Comment

 
BONYA HAPA