
Na Mwandishi Maalum – Comoro
Ijumaa – Mei 27, 2011
Makamu
wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal alikuwa miongoni mwa viongozi
waliohudhuria sherehe za kuapishwa Rais wa Visiwa vya Comoro Ikililou
Dhoinine ambako alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete.
Sherehe hizo ambazo zimefanyika jana (Alhamisi) kwenye viwanja vya Bunge mjini Moroni zilihudhuriwa pia na Rais wa Madagascar Andry Rajoelina, Makamu wa Rais wa Mauritius, Waziri Mkuu wa Chad pamoja na mabalozi mbalimbali waliowakilisha nchi zao.
Baada
ya kuapishwa viongozi na wageni waalikwa walipata fursa ya kumpongeza
Rais Dhoinine ambaye alishinda nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu
uliofanyika Disemba 27, 2010.
Rais
Dhoinine mwenye asili ya kisiwa cha Moheli anachukua nafasi ya Ahmed
Abdallah Sambi ambaye amemaliza muda wake wa uongozi wa kipindi cha
miaka mitano.
Wakizungumza
katika sherehe hizo Rais Sambi anayeondoka madarakani alielezea
mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha uongozi wake yakiwemo ya
kiuchumi na kijamii wakati kwa upande wake Rais Dhoinine alielezea matarajio yake ya kuleta maendeleo zaidi katika visiwa hivyo.
Wakati
huo huo, Makamu wa Rais Dk. Bilal anaondoka nchini kesho (Jumamosi)
kuelekea Abuja, Nigeria ambako atamwakilisha Rais Jakaya Kikwete kwenye
sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa Nigeria Gooluck Jonathan.
Sherehe
za kuapishwa kwa Rais huyo Mteule wa Nigeria zitafanyika Jumapili
mjini Abuja kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi mkuu wa nchi
hiyo uliofanyika mwezi April, mwaka huu. Makamu wa Rais anatarajia
kurejea nchini Jumatatu ijayo
0 comments:
Post a Comment