TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, May 18, 2011

Auwawa kwa kuiba pikipiki wananchi wakampiga hadi kufa.

6:05 PM



Dereva wa pikipiki al maaruf "bodaboda", Juma Rashidi, 32, mkazi wa Itigi wilayani Manyoni mkoani Singida ameuawa na abiria aliyekuwa anamsafirisha kwenda kijiji cha Tura mkoani Tabora.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida Celina Kaluba  amesema dereva huyo alikatwa kisogoni na kitu chenye ncha kali na  abiria huyo Geu Njongaji na kudondoka chini kisha kuchinjwa shingo.

Mtuhumiwa Geu baada ya kufanikisha mauaji hayo alipora pikipiki yenye namba za usajili T 962 BNF aina ya Sanlag na kukimbia nayo kuelekea kwao kijiji cha Tura. Akiwa anaendesha pikipiki hiyo kwa mwendo wa kasi hakufika mbali kabla ya kugonga shina la mti mkubwa na kuumia vibaya. Akaamua kurudi Itigi kwa ajili ya kupata matibabu katika hospitali ya misheni ya St. Gasper. Wananchi waliokuwa wameshapata taarifa ya dereva wa bodaboda kuuawa walipomwona, walimvamia na kuanza kumpiga.

Geu aliweza kupenya na kuwatoroka kwa kukimbilia katika chumba cha walinzi wa benki ya NMB Itigi kwa lengo la kujisalimisha. Wananchi wakawashinikiza Askari waliokuwa lindoni wamtoe Geu lakini Askari hao hawakukubaliana na ombi lao. Ndipo wananchi walipofanya fujo kubwa na kuharibu milango, madirisha na vioo vya magari na kufanikiwa kumtoa Geu ambapo walimpiga kwa silaha mbalimbali hadi alipokata uhai.
Kamanda Kaluba amesema polisi inawashikilia Mohammed Masoud (24) na David Nicodemo (25)kuhusiana na mauaji hayo na kuharibu mali ya benki.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA