![]() |
| Chelsea imemtimua meneja wake Carlo Ancelotti baada ya kumaliza msimu wake wa pili bila kombe lolote. |
Alitimuliwa baada ya Chelsea kumaliza Ligi msimu huu kwa kuchapwa bao
1-0 na Everton na klabu hiyo ikimaliza kwa kushika nafasi ya pili ya
msimamo wa Ligi Kuu ya Soka ya England.
Ancelotti mwenye umri wa miaka 51 mkataba wake ulikuwa umalizike mwakani katika klabu ya Chelsea.
Taarifa ya klabu hiyo imesema: "Matumaini yetu
kwa msimu huu yamekuwa mabaya kutokana na matokeo tuliyopata tofauti na
tulivyotarajia na klabu inaona ni sawa kabisa kufanya mabadiliko haya
kwa ajili ya maandalizi mazuri ya msimu ujao."
Wameshindwa kubeba kombe la Ubingwa wa Ligi na
kuikodolea macho Manchester United ikichukua kombe hilo kwa mara ya 19
wiki moja iliyopita, pia Chelsea wakatolewa katika mbio za kuwania
Ubingwa wa Vilabu kwa nchi za Ulaya, wakatupwa nje kombe la FA na
vilevile kuwania Kombe la Carling msimu huu.
Chelsea ambao walikuwa mabingwa watetezi wa Ligi
Kuu na Kombe la FA msimu huu uliopita, wamemaliza pointi tisa nyuma ya
Manchester United na wamewatangulia Manchester City walioshika nafasi ya
tatu kwa tofauti ya mabao tu.
Meneja wa zamani wa klabu hiyo Avram Grant naye
alikumbana na hali kama hiyo wakati Chelsea ilipomaliza nafasi ya pili
katika Ligi Kuu ya England na ikashindwa katika fainali ya Ubingwa wa
Ulaya mwaka 2008 kwa mikwaju ya penalti.
Na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich,
aliyemsajili Fernando Torres kwa kitita cha paundi milioni 50 wakati wa
usajili mdogo mwezi wa Januari, sasa ataanza hekaheka za kumpata meneja
mwengine mwenye uwezo wa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu kutoka kwa
Manchester United na pia tamaa kubwa ya klabu hiyo ya kubeba kombe la
klabu bingwa ya Ulaya.bbc

0 comments:
Post a Comment