Mwana mfalme William akifungishwa ndoa na Aksofu Rowan William katika kanisa la Westminster Abbey jijini London.
Maharusi hao walishangiliwa na maelfu ya watu
waliojipanga barabarani kuelekea kasri ya Buckingham Palace ambako
Malkia amewaandalia karamu wageni 650.
Wana ndoa hao wapya walitumia gari liliovutwa na
farasi la muundo wa mwaka 1902 ambalo lilitumiwa na wazazi wake Prince
William wakati wa ndoa yao mwaka 1981.
Maharusi hao baadaye walijitokeza kwenye roshani ya kasri ya Buckingham na kuwasalimu maelfu ya watu waliokwenda kuwasherehekea.
Baada ya kulishana viapo vya ndoa Askofu mkuu wa Canterbury, Rowan Williams, aliwanadi rasmi kuwa "mume na mke".
Kuanzia sasa maharusi hawa watajulikana rasmi kama Duke na Duchess wa Cambridge. |
0 comments:
Post a Comment