Kampuni
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imekamilisha
mashindano ya kuchoma nyama katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha ambapo
yamefanyika kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa
mwitikio mkubwa wa wananchi wa mikoa hiyo Akizungumzia fainali
hiyo ya aina yake, Meneja wa Bia ya Safari lager Fimbo Butallah alisema
fainali za mwaka huu katika mikoa hiyo zimekuwa za kufana na kwa
mafanikio makubwa jambo ambalo limepelekea kufanikiwa kwa malengo ya
safari larger katika kuasisi na kuendesha mashindano hayo Alisema
lengo kuu la mashindano hayo ni kuwezesha maboresho katika maeneo ya
baa na pia kusaidia kukuongeza ujuzi kwa wachoma nyama ili kuwezesha
wanywaji wa beer za safari kupata fursa ya kula nyama choma bomba huku
wakishushia na safari lager baridi Katika kufanikisha haya beer
ya safari iliweza kuwatafuta majaji mahiri waliobobea katika maswala ya
utayarishaji,uchuaji wa nyama na uchomaji ambao wamepata utaalam wao
katika nchi mbalimbali zilizobobea kwenye taaluma hiyo Kwa
upande wao wakuu wa mikoa ya Arusha na Kilimanjaro katika hutuba zao
zilisomwa kwa niaba yao na wawakilishi wao walisema serikali
itahakikisha inawasaidia na kuendeleza juhudi za bia ya safari katika
kuhakikisha wanywaji wa beer wanapata nafasi ya kula nyama choma bomba
huku wakiwataka baa zote zilizofanikiwa kuingia kwenye hatua ya tano
bora kwa mioa hiyo kuendeleza ubora wa uchomaji wa nyama ili kuweza
kuhakikisha wanabakia katika nafasi za ubora walio nao kwa hivi sasa Mahindano
ya hayo mkoani Arusha yalishirikisha baa za Songambele ambao ni
washindi wa kwanza, sakina baaa washindi wa pili,Angels pub washindi wa
tatu, Arusha Night Park washindi wan ne na washindi wa tano ni QX Pub
ambapo fainali zake zilifanyika katika viwanja vya AICC Club huku mkuu
wa mkoa hua akiwakilishwa na meya wa Jiji hilo Bwana Lyimo Mkoani
Kilimanjaro baa zilizoingia hatua ya tano bora ni Makanyaga bar ambao
ni washindi wa kwanza, East Africa bar washindi wa pili, Mkulima Bar
washindi wa tatu,Green Garden bar washindi wan nne na White star
washindi wa tano ambapo fainali zilifanyika katika Hotel ya Hugos
iliyopo mjini Moshi Aidha fainali hizo zilipamwa na burudani
toka katika bendi za Ndanda Cosovo na Family bend ambazo ziliweza kutoa
burudani murua kwa maelfu ya wapenzi wa beer na nyama choma
waliofurika katika fainali hizo ambapo fainali mkoani Arusha ilikuwa
jumamosi ya 26/03/2011 na mjini moshi ni jumapili ya 27/03/2011
|
0 comments:
Post a Comment