TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, July 5, 2010

JK akagua Faru Serengeti

12:54 AM

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Huduma ya maji kwa Jamii Mhandisi Frida Rweyemamu(watatu kushoto) akitoa maelezo ya mradi wa maji jana wakati Rais Jakaya kikwete(katikati) alipokagua bwawa kubwa la maji katika mji wa Mugumu wilayani Serengeti jana.Kushoto ni Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.Rais Kikwete ameshauri mradi wa ufugaji samaki na uvuvi ufanyike katika bwawa hilo. JK akisalimiana na baadhi ya wananchi wa mji wa Mugumu waliojitokea kumlaki wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti. JK na Waziri wa Maji profesa Mark Mwandosya na Mbunge wa Serengeti Dr.Wanyancha wakijadiliana jambo wakati wa ufunguzi wa mradi wa maji katika Mji wa Mugumu,wilayani Serengeti
JK akiwapongeza vijana wadogo wawili Brittany Scalciewicz(10) na kaka yake Joey Scalciewicz kutoka jimbo la California nchini Marekani ambao wako nchini Tanzania kwa utalii na walifanikiwa kupanda na kufika kilele cha mlima Kilimanjaro hivi karibuni.Vijana hao wadogo pamoja na wazazi wao wanaitembelea mbuga maarufu ya Serengeti ma walikutana na Rais Kikwete katika uwanja wa ndege wa Seronera,wilayani Serengeti wakati Rais Kikwete alipokwenda kuzindua mradi mkubwa wa maji katika mji wa Mugumu jana JK akikagua moja wa faru weusi(black rhino) waliorejeshwa nchini kutokea Afrika ya Kusini hivi karibuni katika makazi yao ya muda huko mbuga ya Serengeti.Faru hao baadaye wataachiliwa na kuishi katika mazingira ya asili.Rais Kikwete aliwakagua faru hao wakati alipokuwa njiani akitokea mji wa Mugumu wilayani Serengeti ambapo alizindua mradi mkubwa wa maji na kuongea na wananchi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA