TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, June 20, 2010

MHESHIMIWA WAZIRI KAMALA, AONGEA NA WATANZANIA WAISHIO UINGEREZA

1:53 AM

Mheshimiwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala (akihutubia) Ijumaa 18 Juni 2010 amekutana na Watanzania waishio Uingereza kwa lengo la kuwafahamisha wananchi hao masuala mbalimbali ya Utangamano wa Jumuiya hiyo.

Ziara ya Mheshimiwa Dk. Kamala inatokana na ombi la wananchi hao kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda alipotembelea London mwezi Mei mwaka huu. Mheshimmiwa Pinda aliwaahidi wananchi hao kumtuma Dk. Kamala kuja kutoa ufafanuzi kuhusiana na maendeleo na mapatano yaliyofikiwa katika Jumuiya hiyo.

Mmkutano huo ulifanyika katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania, London. Mikutano mengine miwili ya Waziri huyo na Watanzania itafanyika katika miji ya Reading leo Jumamosi, 19 Juni 2010 na Manchester ni kesho Jumapili, 20 Juni 2010, yote kuanzia saa kumi jioni.

Hotuba kamili ya Mheshimiwa Waziri itatangazwa kwenye tovuti ya Ubalozi baadae.


Mheshimiwa Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala, (pili kushoto), Mheshimiwa Balozi wa Tanzania hapa nchini Uingereza, Mama Mwanaidi S. Maajar, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania hapa Uingereza, Bwana John Lusingu na Mwakilishi kutoka Jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.

wadau wakifuatilia hotuba ya waziri
wengi walijitokeza kumsikiliza Dk. Kamala




0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA