
Hakuna anayeweza kuamini. Ni maruweruwe matupu.
Wandaaji wa michuano ya kombe la dunia la mpira wa miguu, Afrika Kusini, wamepokea kipigo cha magoli 3-0 kutoka kwa mabingwa wa kwanza wa kombe la dunia Uruguay.
Bao la dakika ya 24 la krosi ya mbali kabisa nje ya boksi liliwaharibu Bafana kisaikolojia.
Kipindi cha pili kikashuhudia golikipa wa Bafana akitolewa kwa kadi nyekundu huku akiwazawadia penati Uruguay ambao waliitumia vema.
Bao la sekunde za mwisho, likapigilia msumari wa moto kwenye kidonda cha Waafrika.
0 comments:
Post a Comment