TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, May 17, 2010

Mwafaka wapatikana KKKT

2:08 PM

Mgogoro uliozuka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Makoka jijini Dar es Salaam, umemalizika baada ya pande zote kuafikiana.

Mwafaka huo ulipatikana jana baada ya baadhi ya viongozi wa kanisa kukiri makosa kisha ikafanyika sala ya toba.

Msaidizi wa Askofu wa Kanisa hilo Mashariki na Pwani, Jeorge Fupe, ndiye aliyeongoza shughuli hiyo.

Gazeti hili lilifanikiwa kufika katika eneo la kanisa na kuwashuhudia waumini wakiwa wametulia kutaka kujua hatma ya mgogoro huo.

Fupe aliwaomba waumini na wazee wa kanisa hilo kurejesha amani, kufuatia vurugu zilizozuka Jumapili ya Mei 9, mwaka huu na kukwamisha misa.

Katika mahubiri yake, Fupe alisema kitendo hicho kilichofanywa cha kuvuruga amani ya kanisa pamoja na kuvunja ibada sio kizuri na kwambani dhambi.

Fupe alisema waliofanya vurugu hizo wanatakiwa kutubu dhambi zao ili kurudisha amani ya kanisa kwani tukio hilo lilionyesha taswira mbaya kwa jamii.

Baada ya kauli hizo, wazee kadhaa walijitokeza na kuomba ifanyike sala ya toba na kwamba nafsi zao zimewasuta kwa makosa waliyoyatenda.

Kila mmoja alikiri kosa na hatimaye kufanyika sala ya toba na kuahidi kutorudia kosa walilolifanya.

“Ni kweli nilifanya vurugu pamoja na wenzangu huku nikiwa ninafunga mlango kumzuia mwinjilisti asiingie kanisani ila imenibidi nije ibada hii ya pili kwani awali roho yangu ilikuwa inanisuta kwa yale niliyoyafanya na hivyo naomba niongozwe sala ya toba,” alisema muumini mmoja.

Hata hivyo Fupe alipomaliza kuongoza sala ya toba aliendelea na ibada na kuwasisitizia waumini kuwa na upendo.

Mmoja wa waumini aliyezungumza na gazeti hili, alisema chanzo cha mgogoro huo ni wazee kadhaa wa kanisa kutopendezwa kukosolewa na mwinjilisti Nistisile Makarious baada ya kugundua kuwa walitenda makosa.

Tofauti na ilivyokuwa Jumapili ya Mei 9, jana hapakuwepo na askari polisi katika eneo la kanisa hilo.

Katika vurugu hizo, wazee wa kanisa na waumini kadhaa walimzuia Mwinjilisti Makarios asiongoze ibada na kuwalazimisha polisi kufika.

1 comments:

SHAGIHILU said...

du afadhali yameiisha. kinachonisikitisha katika nyakati hizi binadamu hatutaki kukosoana. mtu akikosolewa tu kosa la jinai. duh! thanks for the info i have been waiting to here. thanks.

Post a Comment

 
BONYA HAPA