
Rais wa Kenya na waziri mkuu wamekutana kwa mara ya kwanza, tangu uzuke mvutano kati yao wiki moja iliyopita uliotishia serikali ya muungano nchini humo.
Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga wamekutana katika ofisi ya rais mjini Nairobi.
Wawili hao walihitilafiana baada ya Rais Mwai Kibaki kupindua uamuzi wa Waziri Mkuu Raila Odinga wa kuwasimamisha kazi mawaziri wawili kwa tuhuma za ufisadi.
Kibaki na Raila waliunda serikali ya pamoja ili kumaliza machafuko yaliyofuatia uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Hata hivyo muungano huo umekuwa katika hali tete.
0 comments:
Post a Comment