Watoto wawili mtu na mdogo wake wamenusurika kifo baada ya kulipukiwa na bomu linalosadikiwa kuwa ni la kutupa kwa mkono. Aidha mtoto mwingine mwanafunzi wa darasa la sita katika wilaya ya Kishapu naye amepoteza maisha kwa kufa maji wakati akiogelea katika moja ya dimbwi muda mfupi baada ya kupeleka mifugo ya babu yake kunywa maji na yeye kuamua kuogelea. Watoto walinusurika kifo kwa bomu mmoja ni mwanafunzi wa darasa la nne ambaye amejeruhiwa vibaya kwa bomu hilo walilokuwa wakilichezea kulipuka na kumsababisha kupoteza vidole vyake viwili.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Shinyanga, Daud Sias, alisema juzi mjini hapa kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 3 majira ya saa 8 mchana katika kijji cha Mwamatondo kata ya Nkololo wilayani Bariadi.Mkuu huyo wa polisi mkoani hapa aliwataja watoto waliokumbwa na mkasa huo kuwa ni Saguda Ndongo (11), mwanafunzi wa darasa la nne katika Shule ya Msingi ya Mwamatondo na mdogo wake, Sayi Ndogo, ambaye amejeruhi vibaya usoni na sehemu za mbavu. Akielezea tukio hilo la aina yake kutokea wilayani humo kamanda huyo alisema kuwa siku ya tukio kaka mkubwa wa watoto hao Jija Ndongo (16) aliokota kitu chenye mduara kinachodaiwa kuwa kilikuwa katika mazingira ya nyumba yao na kuanza kulichezea kama mpira.
Aliongeza kuwa kijana huyo na wadogo zake walianza kukichezea na kurushiana kama mpira lakini katika hali isiyo fahamika bado waliamua kwenda kukichoma na ndipo kilipolipuka na kuwadhuru watoto hao ambao wote wamelazwa katika hospitali ya serikali ya wilaya ya Bariadi ya Somanda nje kidogo na mji wa Bariadi.
0 comments:
Post a Comment