TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, December 2, 2009

Ng'ombe wa kafara wazua utata Afrika Kusini

5:56 PM

Mpango wa kuchinja ng'ombe katika kila kiwanja cha soka kitakachotumika kwa fainali za kombe la dunia Afrika Kusini, umezua malalamiko kutoka kwa wanaharakati wa kutetea haki za wanyama.

Kundi la Makhonya Royal Trust, ambalo lilitoa wazo hilo, lilielezea tambiko la kuchinja ng'ombe kuwa "njia muafaka ya kiafrika" kubariki mashindano hayo yatakayofanyika mwaka ujao.

Waziri katika serikali ya nchi hiyo, Sicelo Shiceka ameahidi kusaidia "kupigia debe" wazo hilo mbele ya shirikisho la soka la dunia, Fifa.

Lakini makundi ya haki za wanyama yametaka kushirikishwa kuombwa ushauri kuhusu mipango hiyo.

Mzozo huo umezeka wakati jaji mmoja wa Afrika Kusini alipokataa kuzuia karamu nyingine ya kabila la Zulu kuchinja dume la ng'ombe siku ya Jumamosi, badala yake alisema bunge la nchi hiyo linatakiwa kuamua.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA