England ni miongoni mwa timu 32 zinazosubiri kwa hamu droo inayotolewa siku ya Ijumaa kwa ajili ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zitakazofanyika Afrika Kusini.
Sherehe hizo zinazotarajiwa kuanza saa mbili kamili Afrika Mashariki katika kituo cha kimataifa mjini Cape Town zitashuhudiwa na mamilioni ya mashabiki duniani kote.
Ifikapo mwisho wa kutangaza droo hizo, mataifa yatajua makundi yao ya upinzani na tarehe ya kila mchezo.
Kombe hilo la dunia linatarajiwa kuanza mwezi Juni 11 ambapo fainali itakuwa Julai 11.
Timu za Afrika zilizofuzu kuingia katika kombe la dunia ni Cameroon, Nigeria, Ivory Coast, Ghana, Algeria na wenyeji Afrika Kusini.
0 comments:
Post a Comment