TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Saturday, December 5, 2009

$30 milioni kwa Mshindi wa Kombe la Dunia

12:22 PM
Kamati kuu ya chama cha Soka duniani Fifa imetangaza zawadi ya $30 milioni kwa mshindi wa kombe la dunia Afrika Kusini mwakani.

Katibu mkuu wa Fifa Jerome Valcke alitangaza hayo siku ya alhamisi mjini Cape Town.

Mshindi wa pili atapokea $24 milioni huku kila timu inayoshiriki ikipata $1 milioni kama gharama za maandalizi.

$40 milioni itakuwa kwa vilabu ambavyo wachezaji wake wanashiriki kwenye michuano hayo.

Jumla ya pesa zitakazotolewa kwa timu nchini Afrika Kusini 2010 ni ongezeko la asilimia 61 zaidi kuliko mashindano ya 2006 Ujerumani.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA