Jumuiya ya Afrika Mashariki imeadhimisha miaka 10 huku viongozi wake wakitia saini mkataba wa soko la pamoja la jumuiya hiyo mjini Arusha,Tanzania.
Marais wa Kenya, Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi wamekubaliana kuwepo kwa biashara huru na kuvuka kwa watu kutoka nchi moja hadi nyengine bila ya vizuizi katika eneo lote.
Inatarajiwa kuwa mkataba huo utaongeza ushawishi wa kiuchumi katika eneo hilo.Soko hili la pamoja linatarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka 2010.
Jumuiya ya Afrika Mashariki ilizinduliwa miaka 10 iliyopita na jumla ya idadi ya watu ni milioni 120.
0 comments:
Post a Comment