RAIS Jakaya Kikwete amerudia kuvionya vyombo vya habari nchini visitumie uhuru wao kuvuruga amani na kuvunja umoja wa kitaifa.
Rais Kikwete amesema, endapo vitafanya hivyo Serikali haiwezi kuviacha,vitashughilikiwa.
Sanjari na onyo hilo, Rais Kikwete amesema, Serikali itaendelea kulea na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.
Lakini Rais Kikwete amesema,vyombo vya habari lazima vijirekebishe,vitimize wajibu ambao ni sehemu muhimu ya uhuru huo wa habari.
“Kama nilivyowaambia pale Musoma majuzi wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, huu hauwezi kuwa uhuru wa kuvunja taifa, uhuru wa kugawa watu, uhuru wa kuchochea maasi na ugomvi kati ya dini mbalimbali, kati ya makabila, kati ya watu wenye rangi mbalimbali”
Alisema “Baadhi ya vyombo vyetu havina wajibu kabisa. Vinachochea maasi ya kuvunja nchi na kuleta mfarakano kati ya watu wetu. Vinajaribu kugawa watu wetu, kugawa mataifa yetu na kusababisha maafa makubwa. Hatuwezi kuvumilia vyombo vya habari vya namna hiyo vinavyotumia uhuru kuleta balaa kwa watu.”
Home
»
»Unlabelled
» 'Ole wenu wanahabari mnaovuruga amani'
'Ole wenu wanahabari mnaovuruga amani'
10:02 PM
Mshirikishe Mwezako Kupitia:
0 comments:
Post a Comment