TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Wednesday, November 18, 2009

IPTL yazidi kuongeza umeme gridi ya Taifa

1:07 PM

Mtambo wa nne wa kuzalisha umeme wa Kampuni ya (IPTL), umewashwa na kufanya idadi ya megawati zinazozalishwa na kampuni hiyo kufikia 40.

Kuwashwa kwa mtambo huo kumeongeza kiasi cha megawati zinazoingia katika gridi ya taifa kupitia vyanzo mbalimbali vya kuzalishia umeme kutoka 607 hadi 617.

Mwanasheria wa Wakala wa Ufilisi na Udhamini (Rita), Theophil Rugonzibwa, aliliambia gazeti hili kuwa mtambo huo uliwashwa jana saa tisa mchana baada ya mafundi kuthibitisha kuwa hauna mushkeli.

Alisema mafundi hao baada ya kuwasha mtambo huo wa nne wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha yote inawashwa na kuingiza umeme katika gridi ya taifa.

"Hapa hakuna kulala hadi kieleweke, mafundi wote wako kazini saa 24 ili mradi kufanikisha kuwashwa kwa mitambo yote," alisema Rugonzibwa.

Kuwashwa kwa mtambo huo wa nne wa IPTL,kunafanya idadi ya megawati zinazoingia katika gridi ya taifa kufikia 617 na upungufu wa megawati sasa ni 55.

Shirika la Umeme Nchini (Tanesco), lilisema juzi kuwa mgawo wa umeme unaelekea ukingoni baada ya kubaki na upungufu wa megawati 65 tu.

Akizungumza na Nipashe, Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo, Badra Masoud, alisema mabwawa mengi yaliyokuwa yakikabiliwa na upungufu wa maji sasa yanapata maji ya kutosha na kuzalisha umeme kwa kiwnago kizuri.

Alisema kutokana na hali hiyo hali ya mgawo wa umeme unazidi kupungua siku hadi siku na maeneo mengi sasa yanapata huduma hiyo kwa muda mrefu.

"Hali kwa sasa hivi ni nzuri sana maana watu wanapata umeme wakati mwingi kuliko ilivyokuwa awali kwani uzalishaji katika mabwawa mengi umeongezeka," alisema Meneja Mawasiliano.

IPTLinamitambo kumi na kila mmoja unauwezo wa kuzalisha megawati 10 hivyo itakapowashwa yote itazalisha megawati 100.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA