Mmoja afa, 13 majeruhi na milioni 150 zaporwa katika ujambazi wa mabomu NMB temeke leo
afande wa FFU akiwa na guruneti moja ambalo halikulipuka katika uporaji wa benki ya NMB tawi la Chang'ombe huko Temeke leo.
damu ya wafanyakazi wa katika kaunta ya benki ya NMB tawi la Temeke ambapo majambazi yapatayo saba hivi yalivamia kwa mabomu ya mkono ambapo baada ya kurusha mawili nje na kuua mlinzi wa kampuni binafsi aliyekuwa getini, yakarusha risasi ndani na kujeruhi watu 13, ikiwa ni pamoja na askari polisi wawili na kukomba takriban shilingi milioni 150 kabla ya kutoroka. Walitoroka na Escudo na Prado zilizokuwa na namba za 'SU' na 'STJ'
Hii si mara ya kwanza kutokea uporaji wa aina hii na umekuja siku moja tu baada ya Kamanda wa kanda maalumu ya Dar Afande Selemani Kova kutoa tahadhari kwamba taarifa za kiintelegensia zao zinaonesha kuna kundi la majambazi yenye silaha kali linataka kufanya uhalifu jijini.Tukio kama hilo lilipata kuonekana benki ya za Ubungo, Mwanga na Mbeya.
Mkurugenzi wa Upeleleza wa Makosa ya Jinai afande Robert Manumba akiongea na wanahabari sehemu ya tukio. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Lawrence Masha, Mkuu wa Polisi IGP Saidi Mwema na Mkuu wa mkoa wa Dar Mh. William Lukuvi pia walikuja eneo la tukio baadaye na kutembelea majeruhi waliolazwa hospitali ya Temeke iliyo jirani na Benki hiyo.
Msako kabambe unaohusisha hedikopta, magari, farasi, mbwa na askari wa miguu umeanza toka asubuhi na mapema.
1 comments:
Tenho lido os resumos de suas postagens, porque não estou conseguinda fazer a tradução. Mesmo assim, creio serem todas de relevantes interesses gerais.
Abraços, boa semana.
Post a Comment