TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, July 19, 2009

Wagonjwa wa moyo kwenda India kupungua mwakani

2:38 PM
http://www.loc.gov/rr/international/asian/images/india_flag.gifFredy Azzah na Anna Lusana

SAFARI za Wangonjwa wa Moyo kwenda nchini India, zinatazamiwa kupungua baada ya kukamilika kwa ujenzi wa hospitali ya moyo inayojengwa kwa msaada wa serikali ya China.

Akizungumza jana na Mwananchi Jumapili baada ya kusaini mkataba wa ujenzi wa hospitali hiyo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni alisema hospitali hiyo itakuwa na uwezo wa kulaza wangonjwa 100 kwa wakati mmoja.

“Hospitali hii itakuwa mkombozi kwa watanzania kwa sababu kiukweli hatuwezi kupeleka wagonjwa wote India, wagonjwa watapata matibabu kwa wakati. Ujenzi unaanza mara baada ya kusaini mkataba huu,” alisema Nyoni.

Alisema hospitali hiyo itajengwa kwa muda wa miezi 14 na itakuwa na kitengo cha kufundishia wataalam wa moyo.

Hospitali hiyo inayojengwa ndani ya eneo la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, itagharimu yen za China 63.5 milioni ambazo ni sawa na Sh6.3 bilioni.

Alisema ujenzi huo utasimamiwa na kampuni ya kichina (Shandong and technical group).

Alisema serikali ya Tanzania itachangia kwa kusamehe kodi vifaa vyote vitakavyo ingizwa nchini kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na gharama zitakazo ongezeka ambazo hazikuwamo katika mkataba.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA