Hofu ya Rais al Bashir ilianza wakati wa ziara ya mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Moreno Ocampo nchini Uganda.
Bwana Ocampo alikutana na viongozi na kujadili kesi inayomkabili kiongozi huyo wa Sudan.
Waziri wa mambo ya nje Okello Oryemo aliwaambia waandishi kwamba wanayo hati ya kumkamata Rais Bashir endapo atakanyaga guu nchini Uganda hata ikiwa amealikwa kuhudhuria mkutano.
Muungano wa Afrika
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la Sudan, Suna, Rais Museveni alikanusha matamshi ya waziri huyo na akampigia simu mwenzake kumwomba radhi. Tangu hati ya kumkamata kutolewa mwezi Machi, Rais Bashir ameweza kutembelea nchi kadha barani Afrika.Uganda imetia saini mkataba wa ICC na inawajibika kutekeleza maamuzi yake.
Lakini Uganda pia ni mwanachama wa muungano wa Afrika AU, ambao katika mkutano wa marais uliofanyika nchini Libya mapema mwezi huu, walikubaliana kutoiheshimu hati hiyo.
Rais Bashir anashutumiwa na mahakama hiyo kwa kuandaa mashambulizi dhidi ya raia katika jimbo la Darfur.
0 comments:
Post a Comment