TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Sunday, July 19, 2009

Mtoto amua mwenzake kwa bunduki

2:52 PM
http://mario239303.files.wordpress.com/2008/09/gun.jpg
Na Hussein Semdoe, Handeni

MTOTO Hashiruna Hassan (5) ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Awali ya Suwa iliyopo katika Kijiji cha Suwa Kata ya Mazingara wilayani Handeni , amekufa baada ya kupigwa risasi na dada yake Mwanaidi Hassani (8).

Mwanaidi alimpiga Hashiruna risasi hiyo kichwani sehemu ya jicho kwa kutumia bunduki ya baba yao aina ya gobore wakati walipokuwa wakiichezea nyumbani kwao.

Akizungumzia suala hilo Afisa Mtendaji wa kata hiyo, Hassani Lugundi alisema tukio hilo lilitokea saa 4:00 usiku wa kuamikia jana.

Mgundi alisema wakati tukio hilo likitokea baba yao hakuwepo nyumbani kwake. Alisema kuwa tayari polisi wilaya ya Handeni walifika jana katika eneo la tukio.


0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA