TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA KWA BEI NAFUU / ADVERTISE YOUR BUSINESS HERE AT CHEAP RATES | CONTACT ME: kilinyepesi@gmail.com

 photo DTB_zps7bd2662d.jpg

 photo fl_zps09337f7a.jpg


Habari Mpya:
Monday, July 20, 2009

Mfanyakazi wa ubalozi aachiliwa Iran

2:27 AM


Iran imemuachilia kwa dhamana mfanyakazi wa mwisho wa ubalozi wa Uingereza ambaye ilikuwa inamzuia, kati ya wafanyikazi tisa, kufuatia malalamiko kupinga uchaguzi wa urais mjini Teheran, mwezi uliopita.

Alikuwa ni kati ya wafanyakazi tisa wa ubalozi mjini Tehran, ambao walikuwa wanashtakiwa kwa kuchochea ghasia na malalamiko kupinga kuchaguliwa tena kwa Rais Mahmoud Ahmadinejad.

Mtu huyo, ambaye ni mdadisi mkuu wa masuala ya kisiasa, anatazamiwa kufikishwa mahakamani hivi karibuni.

Uingereza inakanusha madai ya serikali ya Tehran kwamba wafanyakazi wa ubalozi wake walichangia katika kuchochea hali ya ghasia nchini humo na kusababisha maandamano ya watu wengi.

Mgombea urais wa upinzani, Mir Hossein Mousavi, anasema udanganyifu ulifanyika katika uchaguzi huo, katika kuhakikisha Bw Ahmadinejad alitangazwa mshindi.

Rais na tume inayohusika na uchaguzi huo, ilitupilia mbali madai hayo.

0 comments:

Post a Comment

 
BONYA HAPA